Showing posts with label ANOUNCEMENTS. Show all posts
Showing posts with label ANOUNCEMENTS. Show all posts

Jobstanzania Fans Rewards this December


are you a jobstanzania.org fans...?
sasa mwezi wa 12 ndio ule mwezi wa pongezi zetu kwa fans wetu. tutatoa zawadi kem kem kupitia ukurasa wetu wa facebook.

ilikushiriki join our facebok page now. na ufurahie mafanikio yetu pamoja nasi.

Eid Mubarak Kutoka Kwa Timu Nzima Ya Jobstanzania.Org


Napenda Kuchukua Nafasi Hii Kuwatakia Wadau Wote Wa Jobstanzania.Org  A Happy Eid-Al-Fitr,  Na Kwa Wale Walioweza  Kitimiza Nguzo Hii Muhimu Ya Kufunga  Katika Mwezi Huu Wa Ramadhani Basi Naomba Mwenyezi Mungu Azikubali Funga Zenu  Na Dua Zote, Mwenyezi  Mungu Awazidishie Mema Ya Duniani Na Funga Zenu Ziwe Za Kheri, 

Sherekeheni Siku Kuu Hii Kwa Amani Na Upendo, Na Kufanya Yale Yote Yanayo Mpendeza Mwenyezi Mungu. Tunakutakia Eid Mubarak Kwa Wewe Na Familia Yako Na Mwenyezi Mungu Awabariki Na Mpate Barakah (Baraka) Katika Dunia Na Akhirah (Akhera).

Eid Mubarak Kutoka Kwa Timu Nzima Ya Jobstanzania.Org

Nafasi za Mafunzo na Kazi (VOLUNTEERING TRAINING OPPORTUNITIES)


VOLUNTEERING TRAINING OPPORTUNITIES " NAFASI ZA MAFUNZO NA KAZI "

RafikiElimu   Foundation  wanatangaza  nafasi za  mafunzo  ya  ujasiriamali .  Mafunzo  yatakayo  tolewa  ni  pamoja  na  :
1.   Kutengeneza  sabuni
2.  Kutengeneza    chaki
3.Kutengeneza  mishumaa.
4.Kutengeneza   viatu  vya  ngozi.
5. Kutengeneza  mkaa  kwa  makaratasi.
6. Kutengeneza  batiki.
7. Uokaji  mikate
8. Usindikaji  wa   vyakula  na  vinywaji  pamoja  na
9.  Uongozi  wa   biashara.

WALENGWA   WAKUU  WA  MAFUNZO/  SIFA  ZA   WASHIRIKI
Ili  uweze  kupata   nafasi  ya  kushiriki  katika  mafunzo  haya  unatakiwa  uwe  na  sifa  zifuatazo:
1.  Uwe  raia  wa  Tanzania.
2. Uwe  na  umri  wa  kuanzia  miaka  16  na kuendelea
3. Uwe  unajua  kusoma  na  kuandika .

ADA  YA  KUSHIRIKI  KATIKA  MAFUNZO
Ada  ya  kushiriki  katika  mafunzo  haya  ni  shilingi   Elfu  Ishirini  na  Tano  Tu (  Tshs.  25,000/=)

MALIPO  YA  ADA
Malipo  ya  ada  ya  mafunzo  yafanyike  kupitia   CRDB  BANK,  Account  number0152395997900 ,   Jina  la  Akaunti  ni    RAFIKI  ELIMU FOUNDATION.


             Malipo  yafanyike  kabla  ya  tarehe   28  Agosti  2012

            TAREHE  YA      KUANZA  KWA  MAFUNZO
 Mafunzo  yataanza  rasmi  siku  ya  tarehe  01  Septemba  na  yatafanyika  katika  vituo  vya   Dar  Es  salaa,  Arusha, Moshi, Mwanza, Tanga, Morogoro,Mbeya   na  Dodoma.


                    NAFASI  12  ZA  KAZI
Washiriki  kumi na  wawili   ( 12  )watakao  fanya  vizuri  katika  mafunzo  haya  watapata  nafasi  ya  kufanya  kazi  na  asasi  katika    mradi  wa    Elimu  Ya   Ujasiriamali  Mijini  na  Vijijini  " EUMIVI  Project "  utakao  anza   mwezi  Novemba  2012  hadi  Novemba  2014.

Kujiandikisha   katika  mafunzo  haya,  tuma  barua  yako  ya  maombi  , ikiambatana  na nakala  ya  cheti  chako  cha  kuzaliwa  ama   nakala  ya  kadi ya  mpiga  kura, pamoja  na  nakala  ya  risiti  ya  malipo  ya  ada  ya  mafunzo    kwenda  kwa  :

Mkurugenzi  Mtendaji,
RafikiElimu   Foundation,
S.L.P  35967,
Dar  Es  salaam.


Mwisho  wa    kupokea    maombi  ni  tarehe   28  Agosti  2012.

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI



KUITWA KWENYE USAILI
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Halmashauri ya Wilaya ya Babati, Local Government Training Institute - Hombolo (LGTI), Institute of Rural Planning Dodoma (IRDP), Cooperative Audit and Supervision Corporation (COASCO), Tanzania Official Seed Certification Institute (TOSCI), Tanzania Atomic Energy Commission (TAEC) na Taasisi ya Sanaaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) anatarajia kuendesha usaili na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi, waombaji watakaofaulu usaili.
Wasailiwa wanashauriwa kuzingatia yafuatayo:
1. Kuja na vyeti Halisi (original certificates) za kuanzia kidato cha nne, sita, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za mwombaji.
2. “Transcript”, Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
3. Kila msailiwa aje na picha moja (Passport size).
4. Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi.
5. Kila msailiwa azingatie tarehe na eneo alilopangiwa
6. Kila msailiwa aje na cheti halisi cha kuzaliwa (Original Birth Certificate)
7. Wale ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa maombi yao hayakufanikiwa na wasisite kuomba mara nafasi za kazi zitakapotangazwa tena.

Usaili utaanza saa mbili (2:00) Asubuhi na utafanyika katika mahali na tarehe kama inavyoonyesha katika nafasi husika. Wasailiwa wa taasisi kwa nafasi tajwa katika jedwali hapo chini wataanza na mtihani wa mchujo kwanza na kufuatiwa na usaili wa mahojiano kwa watakaofaulu kuendelea katika hatua hiyo.

BOFYA HAPA KWA MAELEZO ZAIDI NA MAJINA YA WALIOITWA

Rest in peace - Steven Charles Kanumba


Rest in peace Kanumba. we gona miss you.... !!!!!

Picture
Steven Charles Kanumba (Januari 8, 1984 - Aprili 7, 2012)


SOMA MAHOJIANO yetu na TANZANIAN BLOGS AWARDS


Kutana Na Mwana blogger wa week hii Ally Msangi


Hello everyone  na karibuni katika mahojiano yetu ya kila week. Week hii tumepata bahati ya kufanya mahojiano yetu na mwanablogger anaye miliki blog ya Jobs Tanzania. 

Karibu sana hapa na tunafurahi sana kufanya mahojiano yetu hapa na wewe. Hebu tuanze mahojiano yetu kwa kuteleza kidogo kuhusu wewe binafsi na blog yako?

Kwa jina naitwa ALLY MSANGI, Ni mwanafunzi wa mwaka wa 3 katika chuo kikuu cha SAUT (St. Augustine University of Tanzania). Nachukua shahada ya kwanza katika masomo ya Biashara (BBA). Blog yangu inajulikana kwa jina la JOBS TANZANIA BLOG ikiwa ni mahususi kwa ajili ya kutangaza nafasi mbali mbali za kazi. Na wasomaji kuweza kuzisoma nakuomba kazi hizo. Blog hii inarahisisha adha ya kuhangaika kununua magazeti kila siku na kuangalia nafasi za kazi, hivyo kwa anae taka kusoma nafasi za kazi zinazo tangazwa anapitia katika blog yangu nakuangalia ni kazi ipi ina mfaa na kuweza kutuma maombi katika anuani husika kwa urahisi zaidi

 
Je, wewe kazi yako ni kublog tu au hii ni kama kazi ya muda tu au hobby?

Ni hobby tu na nina jiskia furaha zaidi ninapotoa huduma hii kwa watu wanaotafuta ajira kupitia mtandao wa internet. Ila hapo mbeleni natarajia kuja kuifikisha mbele zaidi ikiwezekana kufungua RECRUITMENT AGENCY.

Nini changamoto unazozipata kwa kuwa na blog?

Changamoto ninazo zipata ni nyingi sana, ila kubwa ni uelewa wa nini maana halisi ya blog yangu, watu wamekuwa wakidhani kuwa hizo kazi ninazozi post nazitoa mimi hivyo wanajikuta wananitumia vyeti vyao, pamoja na barua za maombi ya kazi hizo n.k. wakidhani mimi ndie muajiri. Nashukuru mungu nimekuwa nikiwaelimisha na sasa kidogo wameanza kunielewa.

Ni miaka mingapi sasa umekua ukiblog?

Ni mwaka sasa tangu nianze ku blog, hapo mwanzo sikutilia maanani kwani sikuona nini faida au umuhimu wa ku blog, nilianza na blog itwayo NIPE5 BLOG  na mpaka leo hii inafanya kazi. Na mwaka huu mwezi wa 05-2011 nilipata wazo lakufungua JOBSTANZANIA BLOG. Hivyo blog hii ya jobs Tanzania ina muda wa takribani miezi mitatu (3) tu.

Ni nani wasomaji wa blog yako?

Wasomaji wakuu wa blog yangu hasa ni vijana walio maliza vyuo na wana tafuta ajira, na wale wote wanao tafuta kazi kupitia mitandao internet.

Je ni mitandao gani mingine ambayo unatumia ili iweze kukusaidia kuitangaza blog yako ili iwafikie wasomaji walengwa wa blog yako? Mfano Twitter au Facebook

Nina tumia facebook kuitangaza blog yangu, unaweza kunipata kupitia facebook page na group page.


Je ni nini mkakati wako na blog yako kwa ujumla?

Mkakati wangu nikui promote blog yangu nakuifanya ifahamike zaidi Tanzania nzima


Je ni bloggers wapi ambao wewe unawaangalia na kufuata nyayo zao? Na kwanini?

Nina pendezwa sana na dada subira wa www.wavuti.com na ndie mtu nae weza kuomba ushauri na akanisaidia nakunijibu, hivyo naweza sema ndio mtu anaenipa hamasa yakuendelea kutoa huduma hii.


Ni nini baadhi ya malengo yako ya mwaka huu kwa ajili ya blogu yako au unaonaje mwenyewe kwa kipindi cha mwaka mmoja au mitano toka sasa hivi blog ya itakuaje?

Nina malengo yakuifanya blog yangu kujulikana zaidi nakuweza kufanya makampuni yaweze kutangaza nafasi zao za kazi kupitia blog yangu bila hata malipo yoyote, pili malengo yangu nikuelimisha vijana wenzangu kuhusu soko la ajira na nini kinachohitajika wanapo tuma maombi ya kazi. Kwani kwa muda huu mfupi nimegundua vijana wengi hukosa kazi kwakuwa hawajui jinsi ya kuandika hata barua za maombi ya kazi (RESUMES, COVER LETER, CV).
Natarajia pia kununua domain ya jobstanzania.com/net/org kama zitakuwa zipo wazi

Je upi ujumbe wako kwa wale watu wanaotaka kuanza kublog?

Blog ni kitu kizuri cha muhimu ni uwe na mtazamo wa nini unachotaka kukitoa kwa jamii kupitia blog yako. Watu wengi huingia katika tasnia hii ya blog kwa kuona mtu fulani ana blog na yeye anataka awe na blog bila kuwa na mtizamo wa nini atakitoa kupitia blog yake.


Asante sana kwa kufanya mahojiano haya na sisi na tunakutakia baraka tele katika masomo yako pamoja na blogs zako.


SHUKRANI ZETU
tuna ushukuru sana uongozi mzima wa TANZANIAN BLOGS AWARDS kwakutupatia nafasi hii ya mahojiano, shukrani sana kwa kuendeleza tasnia hii.


EID MUBARAK FROM JOBS TANZANIA MANAGEMENT


JOBS TANZANIA BLOG TEAM WE'RE WISHING YOU ALL OUR READERS AND VISITORS A LOVELY EIDD EL FITRI,



                                                              OUR MESSAGE
"This is a day which makes us together at one place, creates smiles on all Muslim faces, and increases our love for each other. May we always keep this spirit for each other! 
                                                                  Happy Eid day"

Please DO NOT send any CV or resumes to the owner of this website


Please DO NOT send any CV or resumes to the owner of this website (www.jobstanzania.tk).
We are NOT a hiring firm nor a resume collecting website and neither an employer. Note also that,  we do not have any special connection with any hiring organization and therefore we can not help anybody towards that end.
 

All that we are, is a means to transmit that information 'as is' so you become aware of the available opportunities.

Please read the individual post you are interested in, and obtain the contact information (usually seen at the bottom of the post) where it says,  'How to apply' or 'Contact info' or email and send your credentials to the corresponding address(es) provided. 


We expect that you will carefully read and follow the clearly written instructions.




 KWA KISWAHILI
Tafadali USITUTUMIE maombi wala vielelezo vyako kwa ajili ya kazi. Sisi hatuajiri wala hatuna uhusiano na kampuni ya kuajiri ama yenye kutoa ajira kazi. Matangazo yaliyomo katika tovuti hii ni sawa na jinsi unavyoyaona katika mbao za matangazo au unavyoyasoma matangazo ya nafasi za kazi magazetini, nasi hatuamini kuwa utatundika vielelezo vyako kwenye mbao za matangazo au kuvituma kwenye magazeti,. Hivyo basi, hatutegemei kuwakilishiwa vielelezo vya kazi kwenye tovuti hii vya kuomba ajira.
Tafadhali soma maelezo ya kazi unayotaka, kisha tumia anwani na mawasiliano kama ilivyowandikwa mwishoni mwa kila taarifa ya tangazo la kazi  

TANGAZO LA KURIPOTI KATIKA VITUO VYA KAZI (WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII)


TANGAZO LA KURIPOTI KATIKA VITUO VYA KAZI


KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII, ANAWATANGAZIA WAOMBAJI KAZI WA KADA MBALIMBALI ZA AFYA KUWA WANATAKIWA KWENDA KURIPOTI KATIKA VITUO VYA KAZI WALIVYOPANGIWA MARA WASIKIAPO TANGAZO HILI.


BARUA ZA KUPANGIWA VITUO VYA KAZI ZIMETUMWA KWA WAAJIRI WOTE NCHINI. AIDHA WAAJIRI WOTE MNATAKIWA KUWAPOKEA NA KUWAAJIRI KWA UTARATIBU ULIOPO KATIKA UTUMISHI WA UMMA BAADA YA KUHAKIKI VYETI VYAO.


ENDAPO WAAJIRI MTAHITAJI KUJIRIDHISHA NA MAJINA YA WAHUSIKA MNATAKIWA KUWASILIANA NA WIZARA. AIDHA, MAJINA YA WALIOPANGIWA VITUO VYA KAZI PIA YANAPATIKANA KATIKA TOVUTI YA WIZARA  MAJINA YA WALIPANGIWA VITUO VYA KAZI NI KAMA IFUATAVYO:-



BOFYA HAPA KUSOMA MAJINA

SHUKRANI ZETU KWA WAPENZI WA BLOG YETU


Asanteni sana wapenzi wa blog yetu kwakutupigia kura katika shindado la blogs tanzania. japo hatukufanikiwa kushinda ila tunafuraha kubwa kupata nafasi ya pili na tunaomba mwakani mzidi kutupigia kura zaidi tuwe mshindi wa kwanza

matokeo yalikuwa hivi.

category: Best Advertising/Marketing Blog

www.bongostarlink.com/ 37.5%
http://jobstanzania.blogspot.com 18.18%
http://dartalk.com/ 15.91%
http://infotanzania.blogspot.com 7.95%
http://kingkapita.blogspot.com/ 5.68%
http://ahmed-kidume.blogspot.com/ 5.11%
http://chickabouttown.com/ 3.98%
http://florasalon.blogspot.com/ 3.98%
www.JigambeBlogs.com 1.14%
http://dallyestate.blogspot.com/ 0.57%